Wanahistoria wataka utafiti kufanywa kuhusiana na mti uliotajwa kutumika kama mahakama ya ukoloni

  • | Citizen TV
    367 views

    Wanahistoria kaunti ya Samburu wamependekeza utafiti zaidi kufanywa kuhusiana na mti uliotajwa kutumika kama mahakama ya ukoloni. Mti huu ukitajwa kuwa sehemu ya kutoa hukumu dhidi ya wakenya waliotatiza utawala wa mabeberu. Na kama Bonface Barasa anavyoarifu kutoka kaunti hiyo ya Samburu, mti huo waweza kutumika kama tiba au suluhu kwa kiangazi kinachokumba eneo hilo kutokana na uwezo wake wa kudumu zaidi ya miongo Kumi.