Wanainchi wako na hadi tarehe 14 mwezi huu kuwasilisha maoni yao kuhusu baraza la mawaziri

  • | K24 Video
    64 views

    Wakenya wana hadi tarehe 14 mwezi huu saa kumi na moja jioni kuwasilisha maoni yao kuhusu walioteuliwa na rais William Ruto kuhudumu katika baraza lake la mawaziri. Hii ni kufuatia tangazo lililochapishwa na afisi ya karani wa bunge Serah Kioko, la kukusanya maoni kuhusu maadili ya wateule ishirini na wawili ili kutoa nafasi kwa bunge kuanza shughuli ya kuwahoji na kuwaidhinisha au kuwatema. Wengine watakaofanyiwa tathmini ni mwanasheria mkuu mteule Justin Muturi na katibu mteule wa baraza la mawaziri Mercy Wanjau.