Wanajeshi wa Ukraine wajisalimisha Mauripol huku mapigano yakiendelea maeneo mengine ya nchi.

  • | VOA Swahili
    11,185 views
    Zaidi ya wapiganaji 250 wa Ukraine walijisalimisha kwa majeshi ya Russia kwenye kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol na Kyiv imesema imeamuru wanajeshi wote kuondolewa , na kuelezea ni mwisho wa mapambano makubwa ya umwagaji damu Ulaya katika miongo kadhaa. ............ Kundi la wanawake la Beadwork kutoka jimbo la Samburu limeanza zoezi la kuwafunza wanawake njia mbadala za kujikidhi kimaisha baada ya mabadiliko ya hali ya hewa kuathiri maisha ya wakaazi wengi. Kundi la beadwork huwafunza wanawake hawa kutengeneza shanga na mapambo mengine na kuuza vito hivyo kisha kutumia pesa wanazopata kuendeleza mikakati ya kuhifadhi mazingira pamoja na kuendeleza maisha yao. ......... Hemophilia ni tatizo la kiafya ambapo uwezo wa damu kuganda katika mwili wa mtu huwa ni mdogo sana na kusababisha mgonjwa kuvuja damu nyingi kutokana na kuumia na wakati mwngine bila hata sababu yoyote. Ni ugonjwa wa aina yake wa kurithi ama wakati mwingine kuanza ghafla kwa mtoto aliyezaliwa wataalam wanaitwa mutation.