Wanakandarasi Wajir wadai kutolipwa na serikali ya kaunti

  • | Citizen TV
    Baadhi ya wanakandarasi katika kaunti ya wajir wametishia kufanya maandamano mjini wajir iwapo Serikali ya kaunti hiyo haitawalipa Deni lao katika kipindi Cha wiki mbili zijazo. Wanakandarasi hao ambao tayari wameelekea mahakamani wamedokeza kuwa licha ya kukamilisha miradi tofauti Serikali ya kaunti haijawalipa tangu mwaka wa fedha wa 2018. Hatua ambayo imesababisha baadhi Yao kushindwa kuendelea na biashara zao kwani waliwekeza fedha zote kwenye miradi hiyo. Gavana Ahmed Ali Muktar alipochukua uongozi wa kaunti aliahidi kulipa madeni hayo ya awali kabla ya kuanzisha miradi mingine, hata hivyo miezi kadhaa Baadaye wafanyibiashara hawa wanandelea kulilia haki yao.