Wanamazingira kaunti ya Nyeri wataka upanzi wa miti kudhibitiwa

  • | Citizen TV
    144 views

    Wanamazingira Katika kaunti ya nyeri wameonya wakaazi dhidi ya upanzi wa miti ambayo haijaidhinishwa na Idara ya misitu kama ambayo itasaidia kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Hii ni kufuatia ongezeko la migogoro baina ya majirani vijijini. Agizo hili llilitolewa kwenye hafla ya uhamasisho kuhusu manufaa ya kutunza Mazingira Katika kaunti hiyo. wazazi pia walitakiwa kuwahimiza Watoto wao kupanda miti wakiwa wachanga, Ili kuhakikishia kizazi kijacho kitasaidia taifa kukabili mabadiliko ya tabianchi.