Wanamgambo wa RSF washutumiwa kufanya mauaji

  • | VOA Swahili
    196 views
    Katika makala maalum ya shirika la habari la Reuters inayoangazia mauaji katika taifa la Sudan na hali wasi wasi inaendelea kutanda huko. Awatef Adam, mama wa watoto saba mwenye umri wa miaka 43, alikimbia mauaji ya wiki kadhaa katika mji wa Sudan wa El Geneina hadi Chad katikati ya mwezi Juni, alimuacha nyuma mtoto mmoja wa kiume na wa kike watatu na jamaa na majirani katika jiji hilo na kukimbilia Chad akiwa na mtoto wake mwingine na mabinti wawili. Alikuwa na matumaini hii ingemhakikishia kwamba baadhi ya watoto wake watanusurika. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.