- 13,765 viewsDuration: 28sWananchi Iran wengi wamekusanyika mjini Tehran, wakiwa na bendera na kuimba nyimbo za shangwe baada ya Marekani na Iran kutangaza kusitishwa kwa mapigano kwa muda wa wiki mbili. Iran imekubali kuruhusu usafirishaji salama wa meli kupitia mlango bahari wa Hormuz iwapo Marekani itasitisha mashambulizi yake. Kusitishwa kwa mapigano kunakuja zaidi ya mwezi mmoja baada ya Israeli na Marekani kuzindua mashambulizi dhidi ya Iran, yaliyosababisha Iran kushambulia maeneo mbalimbali katika Ghuba. Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, aliyesuluhisha mazungumzo hayo, alisema kusitishwa kwa mapigano ni 'kunaanza mara moja' #bbcswahili #Iran #Kusitishwakwamapigano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw