Wananchi wa Zimbabwe walalamikia hali mbaya ya uchumi wa nchi yao

  • | VOA Swahili
    99 views
    Baadhi ya raia wa Zimbabwe wanaoishi katika umaskini uliokithiri wanajibu kwa hasira madai ya Rais Emmerson Mnangagwa kwamba uchumi wa nchi unakua kwa haraka katika eneo hilo la kusini mwa Afrika. Mwandishi Columbus Mavhunga anaripoti kutoka Harare, ambako baadhi ya wachumi na wanachama wa chama kikuu cha upinzani wanasema rais hajapewa taarifa sahihi au haelewi misingi ya uchumi.