Skip to main content
Skip to main content

Wanaoishi karibu na msitu wa Maasai Mau wametakiwa kuhama

  • | Citizen TV
    84 views
    Familia zinazoishi kwenye maeneo yanayopakana na msitu wa Maasai Mau wametakiwa kuhama kutokana na mvua nyingi inayoendelea kunyesha. Kamishna wa Kaunti ya Narok Kipkech Lotiatia alikutana na familia zilizoathiriwa na maporomoko ya ardhi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari za mapema mbali na kutoa habari kwa asasi husika kabla ya majanga kutokea. Hata hivyo wenyeji wameelekeza hasira zao kwa wanasiasa wakidai kuwa wanawatelekeza wakati wa shida.