Wanasiasa wa AZIMIO wakosoa mswada wa fedha 2023

  • | Citizen TV
    449 views

    Mbunge wa Saboti Caleb Amisi amewashtumu wabunge wa mrengo wa Kenya Kwanza kwa kukubali kushurutishwa kupitisha mswada wa fedha anaodai una vipengee vinavyonuia kuwalimbikizia wakenya mzigo mzito wa ushuru. Kauli yake imeungwa mkono na mwakilishi wadi wa hospital Eric Mwangale ambaye amesema iwapo mswada huo utapitishwa ataungana na vinara wa AZIMIO kwenye maandamano.