Skip to main content
Skip to main content

Wanasiasa wa upinzani watakiwa kuacha kuwachochea wakenya na serikali

  • | Citizen TV
    967 views
    Duration: 1:48
    Wanasiasa wawili kutoka eneo la Bonde la Ufa wamewataka viongozi wa upinzani, kuacha kuwachochea Wakenya dhidi ya serikali na badala yake kuzingatia kuimarisha umoja na maendeleo. WAkizungumza huko Rongai kaunti ya Nakuru, wakati wa ibada ya mazishi ymbunge wa Kipkelion Joseph Cherorot na Seneta Maalum Jackson Koskei wamesema kampeni za mapema hazina manufaa na zinaweza kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi. Aidha waliwaonya viongozi dhidi ya siasa za urithi wa uchaguzi wa mwaka 2027 mapema, wakisema kuwa Wakenya bado wanatarajia miradi ya maendeleo itekelezwe na serikali ya sasa.