Wanasiasa wapuuza utekaji nyara

  • | Citizen TV
    4,849 views

    Matamshi ya hivi punde ya baadhi ya viongozi kuhusu visa vya utekaji nyara vya vijana vimewakera wakenya hususan wakionekana kupuuza kwamba utekaji nyara umekithiri katika serikali ya rais william ruto na badala yake kuwanyoshea lawama wazazi kwa malezi mabaya ya watoto wao. Huku viongozi hao wakipuuza visa hivyo, familia zimo katika lindi la majonzi na masikitiko.