Wanasiasa wazozana kwenye mazishi katika kaunti ya Nyamira

  • | Citizen TV
    1,778 views

    Hisia zimeendelea kutolewa kufuatia kizaazaa kilichoshuhudiwa wakati wa mazishi eneo a Nyamaiya kaunti ya Nyamira ambapo mgombea kiti cha ubunge cha West Mugirango alifurushwa. Sasa mwanasiasa huyo anayewania kiti hiki kwa chama cha Jubikee Steve Mogaka ameshutumu tukio hilo akiitaka tume ya uchaguzi kuchukua hatua. Kwenye kisa cha hapo jana, inadaiwa kuwa wafuasi wa mbunge West Mugirango Vincent Kemosi wa Ford Kenya walimzuia mwanasiasa huyo kuzungumza na kumuondoa kwenye jukwaa alipokuwa akiwahutubia waombolezaji. Waombolezaji waliojawa na hamaki walimfurusha mbunge huyo kutoka kwenye hafla hiyo