Wanasiasa wazuiwa kutoa semi za kisiasa kwenye mazishi ya mamake Askofu Mkuu Anthony Muheria

  • | Citizen TV
    5,596 views

    Wanasiasa walijipata katika hali ambayo hawajazoea kwenye mazishi ya Mary Agnes Njambi, mamake Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Anthony Muheria na gavana wa benki kuu Dkt Patrick Njoroge huko Kandara, kaunti ya Murang'a. Wanasiasa hawakuruhusiwa kutoa semi za kisiasa kwenye mazishi hayo huku wengi wakitakiwa kuwasalimia waombolezaji na kuketi chini. Gavana wa Murang'a Irungu Kang'ata ndiye mwanasiasa wa pekee aliyeruhusiwa kuzumgumza. Familia ya marehemu ilisema hakupenda siasa mazishini na hivyo ingekwenda kinyume na matakwa yake kwa viongozi kupiga siasa kwenye mazishi yake.