Wanasoka chipukizi DRC wenye ndoto za kwenda kucheza Ulaya.

  • | VOA Swahili
    47 views
    Mjini Goma, mashariki mwa DRC mashindano ya soka ya "Future Pro League" huwaleta pamoja wanasoka chipukizi walio na umri wa chini ya miaka 20, na kuwapa nafasi ya kuonwa na klabu za kimataifa. Tukio hilo, muhimu katika eneo lililoathiriwa na vita kwa takriban miaka 30, linavutia wale wanotafuta vipaji kutoka kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na klabu ya Ligi ya Ufaransa ya AS Monaco.