Skip to main content
Skip to main content

Wanaume wengi wanahofiwa kujitoa uhai Nandi

  • | Citizen TV
    129 views
    Duration: 1:35
    Kamishna wa Kaunti ya Nandi, Wilberforce Kilonzo, ametoa wito kwa wadau kushirikiana ili kuimarisha kampeni za uhamasishaji kuhusu afya ya akili kufuatia ongezeko la visa vya watu kujitoa uhai. Wengi w awaathiriwa ni wanaume katika kaunti hiyo, hali ambayo inazua wasiwasi miongoni mwa jamii. Akizungumza wakati wa hafla ya Huduma Mashinani, Kilonzo alisema kuna haja ya hatua za haraka kuchukuliwa ili kushughulikia changamoto hiyo inayozidi kushika kasi. Alibainisha kuwa msongo wa mawazo unaochangiwa na migogoro ya kifamilia ni miongoni mwa sababu kuu zinazochangia visa vya watu kujiua.