Wanawake wa kanisa la Anglikana lazindua mpango wa kuelimisha umma dhidi ya visa vya kujitoa uhai

  • | Citizen TV
    300 views

    Kutokana na ongezeko la visa vya unyanyasaji wa kijinsia ,mimba za utotoni,visa vya kujitoa uhai na masuala mengine ya kimaadili yanayoibuka katika kaunti ya Nandi,kundi la wanawake kanisa la Anglikana limezindua mpango wa kuelimisha umma dhidi ya kujiingiza katika shughuli zinazotishia maadili ya familia.Mpango huo unayofahamika kama safer communities unalenga kuweka mikakati itakayowezesha jamii mbalimbali kuishi salama.