- 255 viewsDuration: 1:46Wanawake walioko kwenye sekta ya uchimbaji madini kaunti ya Taita Taveta wamepokea mafunzo maalum kuhusu jinsi ya kukabiliana na dhulma za kijinsia wanapoendelea na shughuli za kuchimba madini. Katika mkutano uliowaleta pamoja wanawake kutoka eneo la Kamtonga huko Mwatate ilibainika kuwa ukosefu wa vifaa vya kazi hiyo bado ni changamoto kubwa. Kwa sasa wito umetolewa kwa jamii kuripoti visa vya dhulma za kijinsia hasa baada ya kubainika kuwa wanawake wengi wanahofia kuripoti visa hivyo.