- 566 viewsDuration: 1:15Kinara wa chama cha Safina, Jimi Wanjigi, ametaka uongozi ujao kuheshimu sheria na Katiba, huku ukitoa kipaumbele kwa sera zitakazowawezesha wananchi kujiimarisha kiuchumi. Akizungumza katika mkutano na viongozi wa mashinani jijini Nakuru, Wanjigi amesema taifa linahitaji mabadiliko yatakayowezesha kupatikana kwa uongozi unaowanufaisha wananchi wote badala ya wachache walioko mamlakani.