Wapalestina

  • | VOA Swahili
    125 views
    Majeshi ya Israeli Jumanne yameongeza operesheni zake huko Gaza City licha ya maonyo kutoka kwa viongozi wa Hamas kuwa mashambulizi yanaweza kuathiri mazungumzo yanayoendelea ya sitisho la mapigano. Jeshi la Israeli limesema kuwa wanajeshi wake walikuwa wanapiga katika eneo la Shejaiya na limeuwa darzeni ya wanamgambo. Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN imeelezea wasiwasi wake Jumanne kuhusu operesheni hiyo na amri za hivi karibuni za Israel zimewataka raia waondoke. Shirika la UN lilisema amri hizo zilizotolewa Jumapili ziliwataka raia kuondoka kuelekea magharibi mwa Gaza City kwa usalama wao, na baadaye kushuhudia Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limeongeza mashambulizi yake huko. “Ofisi ya Haki za Binadamu ya UN imerejea kueleza wasiwasi wake kuwa amri ya IDF ikiwataka watu kuhama inakanganya, mara kwa mara ikiwaamirisha watu kuondoka kwenda maeneo mengine ambapo operesheni za kijeshi za IDF zinafanyika. Tunarejea wito wetu kwa Israel kufanya juhudi zote kuhakikisha usalama wa raia huko Gaza,” shirika hilo lilisema katika taarifa yake. Wapatanishi nchini Misri wanajaribu kufanikisha kile kinachotafutwa kwa muda mrefu kusitisha mapigano huko Gaza. White House ilisema Jumatatu kuwa maafisa wa Marekani wako Misri kwa majadiliano yanayolenga kupatika kwa makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas. Wanamgambo wa Palestina waliwauwa takriban watu 1,200 katika shambulizi la kushtukiza na kuwachukua mateka wengine 250 mnamo Oktoba 7, 2023. Shambulizi la kulipiza kisasi la Israel liliofuatia limeuwa zaidi ya Wapalestina 38,000, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo hilo, hesabu yao haitofautishi kati ya wapiganaji na raia. - AP, AFP, Reuters #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen