Wapiga picha wa BBC washindwa kuendelea kupiga pich baada ya kuona jamaa zao Gaza

  • | BBC Swahili
    4,543 views
    Wapiga picha wa BBC huko Gaza wamejikuta wakilazimika kuacha kupiga picha baada ya kupata mshtuko wa kuona marafiki na jamaa zao wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulizi la anga la Israel. Mwandishi wa BBC Adnan Elbursh na mpiga picha Mahmoud Al Ajrami walikuwa wakichukua picha za manusura katika Hospitali ya Al-Shifa wakati majirani zao walipoanza kuletwa miongoni mwa waliojeruhiwa. Mamia ya miili imejaa hospitalini hapo kufuatia mashambulizi ya anga kujibu shambulio la Jumamosi la Hamas ambalo liliua takriban watu 1,300 nchini Israel. - - #bbcswahili #israel #gaza #hamas #Palestine