WASHINGTON BUREAU - MAFURIKO NA JOTO KALI VYAWAATHIRI WAMAREKANI

  • | VOA Swahili
    407 views
    Wiki hii WB inaangalia mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na athari ambazo zimeendelea kujitokeza na hasa hapa Marekani. Ingawa mafuriko ya India , Japan, China , Uturuki pamoja na Marekani huenda yakaonekana kama matukio yanayotokea sehemu mbali mbali za dunia, lakini wataalam wanasema kwamba yanamaingiliano. Hivi sasa hapa marekani kumekuwepo na kipindi kirefu cha joto kali kilichotaanda kuanzia California hadi kusini mwa Florida, na kuwasababisha wataalam wa hali ya hewa wa Arizona kuonya kuwa viwango vya joto vinavunja rekodi katika sehemu hizo. Wakati huo huo mvua zilizopita kiasi zimesababisha mafuriko kweye baadhi ya majimbo ya kaskazini mashariki mwa Marekani, hali inayosemekana ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.