WASHINGTON BUREAU - MDAHALO WA WAGOMBEA MAREKANI WAZUA TAHARUKI

  • | VOA Swahili
    234 views
    Wiki hii tunaangazia mdahalo wa pili wa wagombea urais wa chama cha republican wanaowania uteuzi. Mdahalo huo ulifanyika usiku wa Jumatano kwenye ukumbi wa maktaba ya rais wa zamani Ronald Reagan huko Simi Valley California. Wapinzani wa Donald Trump kwenye chama cha Repablikan walilumbana vikali wakimshambulia rais wa zamani Trump pamoja na wa sasa wa chama cha Demokratik Joe Biden, huku wenyewe pia wakishambuliana kuhusu masuala kama vile China, uhamiaji na uchumi #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.