WASHINGTON BUREAU - RAIS BIDEN NA RAIS XI JINPING WA CHINA WAJADILI UHUSIANO MPYA WA NCHI ZAO

  • | VOA Swahili
    472 views
    Wik hii tunaangazia Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jingping ambao Jumatano wamefanya kikao nje kidogo ya mji wa San Francisco, California pembeni mwa mkutano wa viongozi wa Asia waliokuwa kwenye kongamano lao la kila mwaka la APEC. Mkutano wa moja kwa moja wa Biden na Xi umefanyika karibu mwaka mmoja tangu walipokutana Bali, Indonesia pembeni mwa kongamano lingine la kimataifa. Miongoni mwa masuala muhimu waliozungumzia viongozi hao ni pamoja na tatizo la dawa ya kulevya aina ya fentanyl ambayo inauzwa kwa wingi hapa Marekani kutoka China. Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Marekani ambaye hakutaka kutabulishwa alisema kwamba kudhibitiwa kwa tatizo hilo kutakuwa na athari kubwa kwa walanguzi wa dawa za kulevya kutoka mataifa ya Latin Amerika. Muda mfupi baada ya kikao chao, Biden alisema kwamba, hatua hiyo itaokoa maisha ya watu wengi, wakati akimpongeza Xi kwa kuahidi kukabiliana na tatizo hilo #VOASwahili #biden #xijinping #usa #CHINA