WASHINGTON BUREAU - WAMAREKANI MILION 55 WASAFIRI KATIKA SIKUKUU YA THANKKSGIVING

  • | VOA Swahili
    560 views
    Wiki hii viwanja vya ndege vimefurika wakati watu wakisafiri kwenye sehemu tofauti za nchi ili kuungana na jamaa na marafiki kwa siku kuu muhimu ya shukrani maarufu kama Thanksgiving ambayo huadhimishwa kila Alhamisi ya nne ya Novemba kila mwaka. Inakadiriwa kwamba wamarekani karibu milioni 55 wamesafiri kwa kutumia barabara, ndege na treni, wakati safari za ndege zikisemekana kurejea kwa takriban asilimia 99 ikilinganishwa na 2019 wakati wa kipindi cha janga la Covid-19.#VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.