Washirika wa Gachagua wadai kuna njama ya kumbandua madarakani

  • | KBC Video
    67 views

    Tofauti kati ya naibu rais Rigathi Gachagua na rais William Ruto ilichukua mkondo mwingine leo huku naibu rais akitahadharisha mkubwa wake dhidi ya usaliti. Huku akigusia madai kuhusu njama ya kumbandua madarakani naibu rais, Gachagua alirejelea msimu ambapo rais Ruto alikosolewa vikali, na eneo la Mlima Kenya lilimuunga mkono kwa dhati. Rigathi alimhimiza kiongozi wa taifa kuleta utulivu katika utawala wa Kenya Kwanza huku washirika wake wa kisiasa wakiwapuuza wale wanaodaiwa kuwa watayarishaji wa hoja ya kumg’atua mamlakani.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive