Washukiwa 10 wa dhahabu bandia waachiliwa kwa dhamana ya ya shilingi laki moja kila mmoja

  • | Citizen TV
    199 views

    Hakimu Mkuu mwandamizi Robinson Ondieki amewaachilia kwa dhamana ya shilingi laki moja kila mmoja washukiwa 10 wanaokabiliwa na tuhuma za kufanya biashara bandia ya dhahabu. Ondieki alisema hakuna sababu mwafaka zilizotolewa na wapelelezi wa kitengo cha DCI za kuwazuilia washukiwa hao. Upande wa mashtaka ulitaka kuzuiliwa kwa kumi hao, ili kutoa nafasi ya uchunguzi. Washukiwa walikamatwa kwa kudaiwa kuhusika na biashara hewa na kuwaibia wakenya na hata raia wa kigeni. Mahakama imewaamuru washukiwa kujiwasilisha kwa makao makuu ya DCI kila siku ya Ijumaa.