Washukiwa 2 wa mauaji ya ofisa wa polisi kaunti ya Siaya wapigwa risasi na polisi

  • | Citizen TV
    3,253 views

    Washukiwa wawili wa mauaji ya polisi mjini Siaya wameuwawa kwa kupigwa risasi katika la kijiji cha Hawinga kaunti ya Siaya Jumatano asubuhi. Kamanda wa polisi kaunti ya Siaya Cleti Kemboi amesema kuwa wawili hao walipatikana na bunduki mbili zilizoibiwa Jumatatu katika kisa kilichosababisha kuuawa kwa afisa mmoja wa polisi. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, maafisa wa ujasusi pia wameanza uchunguzi wa uwepo wa kundi la kigaidi kaunti hiyo