- 4,886 viewsDuration: 3:02Mlalamishi aliyelaghaiwa zaidi ya shilingi laki mbili unusu na watu waliojidai kuwa maafisa wa Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) amesimulia jinsi alivyodanganywa na watu hao ambao badala ya kumsajili kwa SHA, walimpora zaidi ya shillingi 280,000 kutoka kwa akaunti yake ya benki. Aidha anasema kuwa matapeli hao pia walichukua mikopo kupitia simu yake. Na kama anavyoarifu Ben Kirui, washukiwa hao wanne walikamatwa Ijumaa na wanasubiri kushtakiwa.