Wasichana kutoka Githurai 44 wapewa bidhaa za usafi wakati wa hedhi, pamoja na mafunzo

  • | Citizen TV
    186 views

    Zaidi ya wasichana elfu moja kutoka mtaa wa mabanda wa Githurai 44 hapa Nairobi wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupokea msaada wa bidhaa mbalimbali ikiwemo sodo ili kujisitiri wakati wa hedhi. Msaada huo umetolewa baada ya wasichana hao kupata mafunzo kutoka kwa shirika la Soles of Africa Girls kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa kudumisha usafi nyakati za hedhi. Jamii eneo hilo imetakiwa kuwa mstari wa mbele kulinda haki za mtoto wa kike dhidi ya dhulma za kijinsia. Aidha serikali imetakiwa kutenga fedha zaidi za ununuzi wa sodo ili kuhkikisha mtoto msichana ako salama dhidi ya mimba za mapema katika mitaa za mabanda Nairobi.