Wasimamizi wa mitihani watakiwa kuwa macho Garissa

  • | Citizen TV
    296 views

    Wasimamizi wa mtihani wa kitaifa katika kaunti ya Garissa wametakiwa kuwa wangalifu na kutoa habari zozote za udanganyifu kwa maafisa wa usalama na baraza la mitihani huo. Naibu kamishina wa Garissa Solomon Chesut amesema kuna tetesi kuwa baadhi ya wasimamizi hao hawazingatii masharti yaliyowekwa na baraza la mtihani ya kutoruhusu mtu yeyote katika vituo vya mitihani. Alisema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale watakaopatikana wakipuuza masharti hayo