Wasiojiweza wapata tabasamu

  • | K24 Video
    33 views

    Shirika binafsi la vijanaambalo lilianzishwa mwaka wa 2015 kwa minajili ya kusaidia jamii zisizojiweza hasa mabandani liliandaa mkutano wa kufadhili wasiojiweza katika hafla nzima ya kuhakikisha wanatimiza ndoto zao katika jamii. Baadhi ya walionufaika na mpango huo hawakuweza kuficha furaha yao, wakisema kuwa kuna haja ya mikakati maalum nchini kwa ushirikiano na wahisani kutoka pembe zote kuhakikisha wanawasaidia wasiojiweza ili wahisi bora katika jamii. Walitoa wito kwa serikali kuendelea kuunga miradi sawia katika jamii ambayo inalenga kuwasaidia wasiojiweza hasa wakati huu ambapo gharama ya maisha ni ghali mno.