Wataalam watoa hamasisho kwa wakaazi wa Taita Taveta

  • | Citizen TV
    183 views

    Kenya ina idadi ya wanawake milioni 16.8 wenye umri wa miaka 15 na zaidi ambao wako katika hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kulingana na utafiti wa Kitaifa kutoka idara ya afya nchini. Makadirio ya sasa yakionyesha kuwa kila mwaka wanawake 5,236 hugunduliwa kuwa na saratani ya shingo ya kizazi huku 3,11 kati yao huaga dunia kutokana na ugonjwa huo. Washikadau wa afya kaunti ya Taita Taveta sasa wako mbioni kuhamasisha wananchi kuhusu ugonjwa huo hatari. Keith simiyu anaungana nasi mubashara akiwa hospitali ya rufaa ya moi, jijini voi.