Wataalamu wa elimu wataka mitaala ya Elimu Afrika Mashariki kuwianishwa

  • | Citizen TV
    180 views

    Wataalamu wa elimu kutoka jumuiya ya afrika mashariki sasa wanashinikiza mataifa wanachama kubuni mtaala wa elimu unaowiana, ili kuboresha viwango vya elimu, Kuendeleza utangamano na kuimarisha uchumi wa jumuiya. Wakizungunza huko Mombasa kwenye hafla ya kuwatuza walimu, wadau wa elimu wamekariri kuwa hatua hiyo itafungua milango katika jumuiya huku wazazi na wanafunzi wakitakiwa kukumbatia mafunzo yanayotolewa na taasisi za kiufundi katika mataifa ya jumuiya ya afrika mashariki. Wadau hao wamesema kuwa hatua hiyo itainua viwango vya elimu. Wameitaka bunge la jumuiya ya afrika mashariki kuanza mchakato huo.