Wataalamu wakumbatia akili dhahania kutibu saratani kaunti ya Kwale

  • | Citizen TV
    40 views

    Wataalamu wa afya katika kaunti ya Kwale wamesema kukumbatia mfumo wa akili dhahania ili kufanya ukaguzi na uchunguzi wa ugonjwa wa saratani kutarahisisha matibabu ya ugonjwa huo. Wakizungumza katika hospitali ya Kinondo ambako kambi ya ukaguzi na matibabu ya saratani bila malipo kwa akina mama yanaendelea, watalamu hao wamesema teknolojia mpya ya ukaguzi inayotumia akili dhahania ina uwezo wa kubaini chembechembe za saratani haraka ikilinganishwa na mfumo wa kawaida wa ukaguzi.