Wataalamu wasema lugha za asili Congo zinapotea kutoka na mchamganyiko wa makabila.

  • | VOA Swahili
    76 views
    Februari 21 kila mwaka, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya lugha za asili duniani ikiwa na makabila 450. Wataalamu wanasema kuwa baadhi ya koo hupoteza lugha zao za asili kwa sababu na mchanganyiko wa makabila au asili. Shirika la Syndicat d'entraide Chrétienne (Muungano wa misaada ya Kikristo) linawahimiza Wacongo kutumia lugha zao za asili huku ikiiomba serikali ya DRC pia kutumia lugha zake nne za kitaifa katika sekta ya elimu. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.