Watangazaji wa Radio Citizen waungana na waumini wa SDA

  • | Citizen TV
    434 views

    Watangazaji wa Radio Citizen waliungana na waumini wa Kanisa la SDA Makongeni hapa jijini Nairobi kwa ibada ya Sabato . Msimamizi wa Radio Citizen, Tina Ogal, alisisitiza umuhimu wa kushiriki katika shughuli kama hizi, akisema ni njia mojawapo ya kuimarisha uhusiano kati ya kituo hicho na wasikilizaji wake mashinani. Haya yanajiri huku Radio Citizen ikiendelea kuongoza katika utafiti kulingana na ripoti ya hivi punde.