Watanzania tisa kati ya 350 waliokuwa Israel warejea Tanzania

  • | BBC Swahili
    3,517 views
    Kundi la watanzania tisa waliokuwa wakiishi nchini Israeli wamerejea nchini kwao hii leo na kupokelewa na ndugu na jamaa katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Hatua yao ya kurejea nchini inakuja wakati mapambano kati ya Kundi la wanamgambo wa Kipalestina Hamas pamoja na jeshi la Israeli yakiendelea. Mpaka sasa Ubalozi wa Tanzania nchini Israeli unasema kuwa hauna mawasiliano na raia wawili wa nchi hiyo ambao wanaishi eneo la kusini mwa Israel ✍@lasteck2023 🎥@Nicholas Mtenga #bbcswahili #tanzania #israel Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw