Watoto katika kaunti ya Samburu huchunga mifugo mchana na kusoma usiku

  • | Citizen TV
    580 views

    Watoto katika jamii ya wafugaji eneo la Barsaloi kaunti ya Samburu,wanalazimika kusoma usiku huku mchana wakiwasaidia wazazi wao kulisha mifugo. Cha kusikitisha ni kuwa masomo hayo yanafikia gredi ya tatu pekee, hali ambayo inawafanya watoto eneo hilo kukosa kuendelea na masomo. Wazazi wanairai serikali kujenga shule eneo hilo ili wanafunzi wapate masomo yatakayowafaidi.