- 349 viewsDuration: 3:33Watoto zaidi wamejitokeza kusimulia masaibu yao ya kulazimika kuwacha shule kwa kukosa karo, licha ya serikali kuwaagiza kuripoti shule bila karo wala sare. Baadhi ya watoto hawa wamelazimika kuwacha shule huku wengine wakisema bado wanangoja kujiunga na Gredi ya 10, wakati wenzao wakiendelea na muhula wa pili. Simulizi hizi zinajitokeza huku Wizara ya Elimu ikikana takwimu za Baraza la Mtihani kwamba wanafunzi zaidi ya laki moja na nusu hawakuendelea na masomo ya mpito wa CBE.