Watu 11 wauawa katika maandamano ya 7/7 Kenya

  • | BBC Swahili
    49,109 views
    Watu 11 wameuawa nchini Kenya katika maandamano ya kuadhimisha miaka 35 ya siku ya saba Saba, kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa muda mchache uliopita. Polisi pia wanasema kwamba watu 567 wamekamatwa ikiwemo mbunge mmoja, huku maafisa 52 wa polisi wakijeruhiwa.