Watu 12 wafariki kwenye ajali tofauti

  • | Citizen TV
    2,132 views

    Watu kumi na wawili waliaga dunia katika ajili mbili tofauti za barabarani Jumatatu usiku, huku wengine zaidi wakijeruhiwa. Katika eneo la Salama katika barabara ya Nairobi kuelekea Mombasa, watu kumi na mmoja walifariki baada ya magari mawili ya abiria kugongana ana kwa ana na lori. Haya yanajiri huku mwanafunzi mmoja wa shule ya upili ya Chavakali pia akiaga dunia papo hapo baada ya basi alimokuwa akisafiria kubingiria katika eneo la Coptic kaunti ya Kisumu.