Watu 13 wafariki kwenye ajali ya barabarani Taita Taveta

  • | Citizen TV
    1,509 views

    Watu kumi na watatu wamefariki na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara ya Wundanyi-Mwatate kaunti ya Taita Taveta. Ajali hiyo ya usiku wa kuamkia leo ilitokea baada ya basi lililokuwa likisafirisha kundi la waombolezaji waliokuwa wakielekea Mombasa kukosa mwelekeo na kubingirika mara tatu.