Watu 2 wafariki na 4 hawajulikani waliko kufuatia maporomoko ya ardhi Mathioya, Murang’a

  • | Citizen TV
    3,962 views

    Watu wawili wamefariki na wengine wanne hawajulikani waliko baada ya nyumba tatu kubebwa na maporomoko ya ardhi katika kijiji cha Kiganjo, eneobunge la Mathioya kaunti ya Murang’a. kwa mujibu wa msimamizi wa idara ya udhibiti wa majanga kaunti ya muranga, Bilha Wanjiku, mwanamume mmoja na wanawe watatu bado hawajulikani waliko. inahofiwa kuwa huenda wamekwama kwenye matope. watu wengine wanne wamenusurika kifo na wanapokea matibabu. shughuli za uokoaji zinaendelea. Maporomoko hayo yalisababishwa na Mvua ukubwa iliyonyesha usiku wa kumkia leo.