Watu 20 wamefariki baada ya kijiji kusombwa na maji ya mafuriko Mai Mahiu

  • | Citizen TV
    6,048 views

    Watu ishirini wamefariki huku wengine wakikimbizwa katika hospitali ya Naivasha kwa matibabu. kwa mujibu wa kamanda wa polisi Naivasha Stephen Kirui, Kijiji kizima cha Kamuchiri kaunti ya Nakuru kimesombwa na mafuriko baada ya mto kijabi kuvunja kingo zake na bwawa kuvunja kuta na kusababisha mafuriko. shughuli ya uokoaji inaendelea. Tukio hilo lilisababisha mafuriko pia kwenye barabara kuu ya Nairobi- Nakuru katika eneo la Maai Mahiu ambapo msongamano mkubwa wa magari unazidi kushuhudiwa. Basi la kampuni ya Easycoach lilijipata kwenye mafuriko hayo na kusombwa na maji. Hata hivyo abiria walikuwa tayari wameshuka kutoka kwenye basi hilo lililokuwa limetoka Narok likielekea Nairobi. wasafiri wameonywa kujihadhari na maporomoko ya mawe.