Watu 3 wafariki kufuatia ajali ya barabarani Limuru

  • | Citizen TV
    768 views

    Watu watatu wamefariki huku wengine wakijeruhiwa vibaya katika ajali iliotokea eneo la Kwambira Manguo kaunti ya Kiambu. Ajali hiyo ilihusisha matatu iliyokuwa ikielekea Nairobi na lori katika barabara kuu ya Nairobi - Nakuru. Haya yanajiri wakati mamlaka ya uchukuzi na usalama barabani NTSA ikiwataka madereva kuwa waangalifu na kutangaza oparesheni haswa msimu wa pasaka unapokaribia.