Watu 3 wakamatwa kwa kuuza mbolea ghushi Nakuru

  • | Citizen TV
    555 views

    Polisi kaunti ya Nakuru wanawazuilia watu watatu kwa tuhuma za kutengeneza mbolea bandia. Watatu hawa wamekamatwa huku baadhi ya wakulima katika eneo la Nyanza sasa wakidinda kuchukua mbolea za ruzuku za serikali wakitaka kufidiwa. Wakulima hawa waliofanya majaribio kubaini endapo mbolea wanayopewa inafikia viwango wanadai kuwa mbolea iliyopo ni bandia.