Watu 3 zaidi wafariki Kitengela na Kirinyaga kutokana na mvua kubwa nchini

  • | KBC Video
    98 views

    Watu watatu zaidi wafarikikatika visa tofauti huko Kitengela na Kirinyaga huku mvua kubwa ikiendelea kusababisha madhara hapa nchini. Huko Kitengela, miili miwili iliopolewa kutoka mtoni na mtaroni, na huko Kirinyaga mwanamke alifariki na wanawe wawili wanauguza majeraha baada ya nyumba yao kuporomoka. Haya yanajiri huku mpasuko kwenye daraja la Kamulu Joska katika barabara ya Kangundo ukiendelea kupanuka ambapo waendeshaji magari walilazimika kupitia kwingineko kufuatia mafuriko kwenye barabara kuu ya Thika karibu na eneo la Kahawa Sukari, kambi ya kijeshi ya Kahawa na chuo kikuu cha Kenyatta. Timothy Kipnusu anaarifu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive