Watu 71 wamefariki kutokana na mafuriko

  • | Citizen TV
    3,233 views

    Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko sasa imefikia 71 huku zaidi ya watu laki moja na hamsini wakipoteza makao. Akizuru kaunti ya mandera hii leo, waziri wa ulinzi Aden Duale aliitaka mamlaka ya ujezi wa barabara nchini kuweka miundombinu inayohitajika ili kurejesha shughuli za usafiri haswa wa vyakula na dawa ambazo zimepungua maradufu kutokana na mafuriko. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, waathiriwa kutoka kaunti za Makueni na Tana River waliirai serikali kuu kuwajengea makao ya kudumu katika sehemu mbadala ili kuepuka uharibifu wa mafuriko ya kila mwaka.