Skip to main content
Skip to main content

Watu kadhaa wakamatwa Mombasa kufuatia maandamano dhidi ya bei ghali ya mafuta

  • | Citizen TV
    1,113 views
    Watu kadhaa wamekamatwa huku shughuli za Uchukuzi wa umma zikikwama baada ya Madereva na wakaazi wa Mombasa kufanya mandamano wakipinga Bei mpya ya Mafuta nchini. Huko Bamburi polisi walilazimilika kuwatimua wandamanaji waliokua wamefunga Barbara na kusababisha kukamatwa Kwa watu watatu waliokuwa miongoni mwa waandamanaji. Hali ya Uchukuzi pia ilisambaratika kati ya Mombasa na mtwapa baada ya wahudumu wa matatu, wananchi na mashirika ya kutetea Haki za kibinadamu kufunga daraja linalounganisha kaunti hizo mbili. Hali hiyo ilipelekea wananchi waliokua wakielekea sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali na viwanja vya ndege kukwama barabarani Kwa saa kadhaa